
Wakazi ameyasema hayo kwenye Planet Bongo inayorushwa na East Africa radio.
"Mi ninavyoona hapa kati kati muziki wa Bongo umekuwa na suala la hype sana na kiki, yani kwamba msanii akitoa nyimbo afanye na kioja na vinakshi nakshi kwamba vitaongelewa", alisema Wakazi.
Akiongelea suala la yeye kuachia nyimbo hivi karibuni, Wakazi amesema toka mwaka jana mpaka sasa amekuwa bize sana na majukumu, lakini hivi karibuni anatarajia kuachia nyimbo aliyomshikisha Damian Soul.
"Suala la kutoa kazi kiukweli mwaka jana hadi hapa saa hizi nadhani nimekuwa bize sana na kufanya kazi nyingi, lakini nikitarajia zaidi kazi ijizungumzie yenyewe badala ya hype, na mwezi wa kumi kati kati kuna nyimbo nyingine inatoka pia, Afro fever featuring Damian Soul, yani kazi zinakuja nyingi na albam zinakuja mbili", alisema wakazi.