
Barnabas ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba kwa msanii mwenye akili anaweza akaanza sasa na kujifunza.
"Mi nafikiri ni msanii mwenye ku tune tu, hapo sio suala la kumlazimisha msanii wala kumuhimiza, msanii mwenyewe mwenye akili na kutumia fikra za mawazo, na kuangalia kipi ni hela", alisema Barnaba.
Pia barnaba amesema kubadilika kwa teknolojia nayo ni moja ya changamoto itakayomfanya msanii kuimba muziki wa band.
"Lakini kiukweli teknolojia na soko la muziki inabadilika, sasa kwa mtu mwenye focus na maono ya mbali, anaweza akaanza sasa, akajifunza na akawekeza sasa, sio lazima, kwa atakaeona inamsaidia kwenye maslahi yake you can do it na akaweza, ukiona haisaidii basi hatuwezi kumlazimisha mtu", alisema Barnaba.
Pamoja na hayo Barnaba amewashauri wasanii wenzake wale ambao hawaimbi muziki wa band, kuanza kuimba muziki huo ili kuendana na soko la muziki lilivyo.