
Kushoto ni Hayati Dkt John Pombe Magufuli, kulia ni msanii Sholo Mwamba
"Baada ya taarifa kutoka nilipokea simu nyingi sana kwamba baba yangu amefariki, kwa sababu ninavyotembea watu wananiita mtoto wa Magufuli ilikuwa ngumu kuamini kama kweli amefariki" amesema Sholo Mwamba.
Sholo mwamba ameongeza kusema Hayati Dkt John Pombe Magufuli alimuachia zawadi ya kitambulisho ambacho anaweza kuingia nacho popote kama msanii kwenye mikutano au ghafla kubwa za viongozi nchini.
Aidha kubwa zaidi atakalolikumbuka kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli ni fedha alizozipata wakati wa Kampeni za kuwania kiti cha Urais, Ubunge na Udiwani ambapo fedha hizo zilimfanya kununua gari lake la kwanza kwenye maisha yake.
Zaidi tazama hapa chini kwenye video.