Master Jay amesema licha ya wana Hip hop wa Bongo kuwa na uwezo mkubwa katika kazi zao za muziki, hawajui namna ya kutumia fursa zinazowazunguka kama wafanyavyo wasanii wa Kimarekani.
“Wana hip hop wa Kimarekani wengi wametumia muziki huo kutengeneza jina na jina lao ndilo lililotengeneza mafanikio yao tofauti na wana hip hop wa hapa Bongo, wanasubiri muziki uwalipe badala ya kuangalia na fursa nyingine kama wanavyofanya Wamarekani,”


