Wasanii watakaowasha moto EATV Awards
Wasanii hao ambao pia wapo wa kutoka Kenya na Uganda, wataandika historia sambamba na tukio kubwa kwenye tasnia ya sanaa Afrika Mashariki EATV Awards.
Hii ndiyo orodha kamili ya wasanii watakao 'perform' na kuandika historia siku hiyo.
- Darassa kutoka Tanzania
- Bill Nass kutoka Tanzania
- Maurice Kirya kutoka Uganda
- Wahu kutoka Kenya
- Lady Jaydee kutoka Tanzania
- Barnaba kutoka Tanzania
- Vanessa Mdee kutoka Tanzania
- Shetta kutoka Tanzania
- Alikiba kutoka Tanzania
Licha ya wasanii wa muziki pia kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo dance kutoka kwa vijana walioshika nafasi tatu za juu katika mashindano ya Dance100 2016 yanayoendeshwa na EATV.
Wasanii hao wameahidi kuangusha show ya nguvu kwa watakaohudhuria tukio hilo, na kuwataka watu wajitokeze kwa wingi kushuhudia wakiangusha mzigo wa nguvu jukwaani.