Wakali wa ‘Amapiano’ Bongo

Jumanne , 8th Jun , 2021

Amapiano ni mtindo wa muziki wenye mseto wa aina mbalimbali za muziki kama deep house, jazz na kadhalika ambao uliibuka nchini Afrika Kusini mnamo 2012 na kusambaa kwenye maeneo mengine ya Afrika. 

Pichani kushoto ni msanii Harmonize, Amber Lulu na Damian Soul

Na hapa nchini kuna baadhi ya wasanii na watayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva ambao wamethubutu kufanya aina hiyo ya muziki pendwa kwa sasa na nyimbo zao zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kufanya vizuri sokoni.

Damian Soul – wimbo wake ‘Mapopo’aliomshirikisha Nhlonipho kutoka Afrika Kusini tangu utoke Disemba 6, 2020 umekuwa ukipata air play karibia kila siku kwenye vituo vya Redio na Tv na sehemu mbalimbali za starehe nchini.

Amber Lulu – ‘Una shingapi’ jam ambayo wengi walipoisikia ikichezwa popote pale walidhani ni msanii wa Afrika Kusini ambaye ameamuwa kutumia lugha ya Kiswahili kwenye uwasilishaji wake wa maudhui kwa hadhira kwani humu amebadilika na kuonesha ukuwaji wake kwenye sanaa.

Wimbo huo umetayarishwa na Daxo Chali pale MJ Records na kuachiwa Januari 4, 2021.

Marioo – ‘Mama Amina’ ilimfungisha safari mpaka Afrika Kusini na kukutana na Sho Madjozi na Bontle Smith wasanii wenye asili yao hiyo ya muziki kisha kupika hit iliyosumbua kila mahali nchini.

Stone Gold – ‘Worry Out’ ni kama kumpiga chura teke kwani ilimuongezea mwendo sana hii kazi msanii huyu ambaye hustle zake hazikuanzia Februari 15 mwaka huu wakati ameachia wimbo huo.

Harmonize – ‘Anajikosha’ tangu Januari 20 mwaka huu ilipotoka track hii bila shaka utakuwa umeisikia mara kadhaa huko kwenye Club  za usiku, Redio na Tv kwani ni moja ya Amapiano kali zilizotoka hapa Bongo.