Alhamisi , 28th Jul , 2016

Country Boy amelazimika kurudia video yake ya 'Aah Wapi', kitendo ambacho kinamaanisha kumuingiza katika gharama za ziada za utengenezaji wa video hiyo.

Country Boy

Country Boy amesema “katika video yangu imeonekana mimoshi mingi tukivuta sigara na shisha, ila idea ya video ilikuwa ni kuonesha kuwa vitendo hivyo sio vizuri. Lakini pia mtu mwingine anaweza akaona na kupotoka kwa sababu mimi ninaonekana na vuta sigara na yeye akajaribu kuiga, Hivyo nimelazimika kuifanyia marekebisho video yangu”.

Country Boy anaamini kuwa kuna watu wengi wanampenda, kumuamini na kumuiga kwani wanampigia simu na kumuambia wanapenda anachokifanya na wanapenda muziki wake pia na sio tu kwa Tanzania bali ni Afrika Mashariki hivyo anajitahidi kuweka maudhui ya kueleweka zaidi katika kazi zake.