Alhamisi , 19th Jun , 2014

Msanii wa muziki Victoria Kimani wa nchini Kenya anazidi kujijengea jina baada ya kuanza rasmi kipindi chake cha maisha ya uhalisia ‘Rise Of The Queen’.

Msanii wa nchini Kenya Victoria Kimani

Hivi sasa dashosti huyo anajiandaa kutoa mixtape yake aliyoibatiza jina “Queen Victoria” kupitia label yake ya Chocolate City ambapo muda wowote kuanzia sasa itaanza kusambazwa kupitia mitandaoni.

Victoria Kimani ameelezea kuwa hivi sasa anazidi kutengeneza episode za kipindi chake hicho kipya akiwashirikisha nyota mbalimbali kutoka nchini Nigeria.