Jumatano , 12th Aug , 2015

Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani, staa wa muziki Vanessa Mdee ametoa ujumbe kwa vijana kutumia nafasi hii kufanya tathmini ya harakati zao katika safari kuelekea kutimiza ndoto zao katika shughuli zao.

staa wa muziki wa bongofleva nchini Vanessa Mdee

Vanessa amesema kuwa, katika wakati huu ambao teknolojia imekuwa kwa kasi, ni nafasi pia kwa vijana kuwa mstari wa mbele kutumia fursa hiyo kujifunza na kujitengenezea mtandao wa ushirikiano katika kuelekea mafanikio yao.