Utovu wa nidhamu wamgharimu Miss Tanzania

Ijumaa , 16th Jul , 2021

Azama Mashango kutoka “The Look Company Limited” ambao ndio waandaaji wa shindano la urembo nchini maarufu kama “Miss Tanzania” ameweka wazi sakata la mshindi wa taji hilo kwa msimu wa mwaka 2020/2 Rose Manfere.

Picha ya Miss Tanzania 2020 na Azama Mashango

Mashango amesema kuwa Miss Tanzania alikiuka baadhi ya vifungu vya mkataba wa makubaliano yao kwa kufanya baadhi ya vitendo vya utovu wa nidhamu hali iliyosababisha kunyang’anywa nafasi ya uwakilishi wa nchi katika msimu wa 70 wa shindano Miss World 2021 na nafasi yake kuchukuliwa na mshindi wa pili, Juliana Lugumisa. 

Baada ya sakata hilo kufika kwenye ofisi za Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), limesema halijaridhia na halijakubaliana na maamuzi ya kumuengua Miss Tanzania 2020/21 Rose Manfere kwenye ushiriki Miss World 2021 mpaka pale kamati ya Miss Tanzania itakapotoa sababu za msingi na kuzithibitisha.

Shindano la Urembo la Dunia (Miss World 2021)linalotarajiwa kuanza kufanyika mwezi Disemba 16, 2021 huko San Juan, Puerto Rico kwenye ukumbi wa Coca-Cola Music.
 

Itazame interview yote hapa