Utabiri mzito wa Peter wa P Square kutimia 2021

Alhamisi , 29th Apr , 2021

Siku ya Mei 5, 2019 msanii kutoka nchini Nigeria aliyekuwa anaunda kundi la P-Square, Peter Okoye 'Mr P' alitabiri kwamba timu za Uingereza zitacheza fainali ya Klabu bingwa Ulaya ''UEFA Champions League'' pia zitacheza fainali ya "UEFA Europa League"

Msanii Peter Okoye 'Mr P'

Utabiri huo ulitimia kwani mwaka huo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilichezwa kwa kuvikutanisha vilabu vya Liverpool ambao walikuwa mabingwa dhidi ya Tottenham Hotspur, kisha ile fainali ya UEFA Europa League ilichezwa kati ya Chelsea waliokuwa mabingwa dhidi ya Arsenal.

Sasa msanii huyo ametabiri tena kuhusu fainali za mwaka huu za michuano hiyo ambapo amesema timu zote za Uingereza zitacheza tena fainali kama alivyotabiri mwaka 2019.

"Ninachoona tena ni fainali nyingine za Klabu za Kiingereza, nilitabiri hii miaka miwili iliyopita na ikatokea hivyo" ameandika Mr P

Kwa sasa timu nne zipo katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambapo Chelsea na Manchester City wapo UEFA Champions League halafu Arsenal na Manchester United wapo nusu fainali ya UEFA Europa League.

Chelsea ilitoka sare ya bao moja ikiwa ugenini dhidi ya Real Madrid nayo Man City ilishinda bao 2-1 dhidi ya PSG ikiwa ugenini, Arsenal na Man United vitashuka dimbani siku ya leo kucheza nusu fainali ya kwanza ya UEFA Europa League.