Jumatatu , 28th Jul , 2014

Baada ya kumaliza usaili wake wa pili wa Dance100% 2014 pale Don Bosco Oysterbay Jumamosi, sasa imebaki nafasi moja tu ya mwisho kwa makundi yenye vipaji vya kudansi Tanzania, kuingia katika mashindano haya kupitia usaili wake wa mwisho.

mashindano ya kucheza ya Dance 100% 2014

Usaili huo mkubwa na wa mwisho utakaofanyika Temeke jijini Dar es Salaam, katika viwanja vya TCC Chang'ombe Jumapili tarehe 3 mwezi Agosti.

Mchongo mzima kuhusiana na kile kilichofanyika Oysterbay na kufanikisha kupatikana kwa makundi matano, utaruka hewani kupitia show kali ya Dance100% ambayo itakujia Jumatano ya wiki hii, kuanzia saa 1 jioni hapa hapa EATV.

Mpaka sasa makundi 10 tayari yamekwisha patikana ambapo yanaingia moja kwa moja hatua ya robo fainali ya mashindano hay0 likiwepo kundi la The Winners Crew, B2K, TWC, Mazabe Powder na Tam Tam Classic na Wakali Sisi, Pambana Fasaha, Quality Boys, Bustani vilevile Tatanisha Dancers.