Jumanne , 22nd Jul , 2014

East Africa Television inakuletea show kali ya usaili wa kwanza wa mashindano ya kucheza muziki nchini Tanzania Dance 100% 2014, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya basketball vya Don Bosco Upanga jijini Dar es Salaam.

Mashindano ya kucheza muziki ya Dance 100% Tanzania

Makundi mbalimbali yalijitokeza kushiriki katika usaili huo wa kwanza ambapo yamo yaliyotokea Mwanza, Kigoma, na mikoa mingine ili kushiriki katika mashindano hayo makubwa ya kucheza muziki nchini Tanzania.

Usikose show hiyo kali ya kusisimua leo kuanzia saa moja kamili jioni ujionee vikundi vilivyoshiriki hadi kufikia hatua ya mchujo na kupatikana makundi matano yaliyofuzu usahili huo wa kwanza.

Zoezi la usahili wa mashindano ya Dance100% 2014 linaendelea kwa kishindo ambapo linaingia kwenye usaili wa pili utakaofanyika Jumamosi hii ya tarehe 26 mwezi huu kwenye viwanja vya basketball vya Don Bosco Oysterbay.

Kama una crew yako ya watu wanne hadi nane kutoka pande zote za Tanzania, mnatakiwa kufika kwa ajili ya usaili huo wa pili utakaofanyika kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa sita mchana.