Jumapili , 9th Mei , 2021

Baada ya kukosekana kwa Tuzo za muziki kwa muda mrefu hatimae Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amethibitisha kurejea kwake mwaka huu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa

‘’Mmekuwa mkililia tuzo na wizara tumejiandaa vizuri katika hili, kuanzia mwaka huu tutaanza kutoa tuzo mbalimbali kulingana na sanaa husika na sekta zote, kwahiyo hili jambo linakuja tushirikiane kuhakikisha kila mwisho wa mwaka maandalizi haya ya tuzo yanaenda vizuri’’.

Tuzo zinaweza kuongeza ushindani, uaminifu wa chapa ya msanii, kujulikana na kujitangaza zaidi.