Ijumaa , 15th Dec , 2017

Kapteni wa Bongo Fleva Tundaman amewataka wasanii waache tabia ya kutoa toa nyimbo kila kukicha wakati nyimbo zenyewe mbovu na hazidumu kwa muda mrefu.

Akiongea na eNEWZ ya East Africa Television, Tunda Man amesema nyimbo zake anazoziandika zinaishi kwa mda mrefu na zinamaudhui yanayojitosheleza kuishi miaka mingi katika sanaa na ndio maana amekaa zaidi ya miaka miwili  tangu ameachia nyimbo yake ya mwisho Mama Kijacho.

Hata hivyo Tundaman anasema pamoja na wasanii wa sasa kuachia nyimbo nyingi kwa wakati mmoja, lakini wengine wanaachia nyimbo ambazo hazina ujumbe wala maana kwa jamii. “Wanatoa nyimbo mbaya ambazo zikipigwa kwenye vyombo vya habari wiki mbili tatu tu mwisho wa siku zinapotea kabisa”.

Tundaman pia ameongelea suala la wasanii kubebwa ambapo amesema katika mziki wa sasa wasanii wamekuwa wanabebwa mara nyingi kwenye vituo mbalimbali vya Radio na Television. Mklai huyo wa 'Hit' kibao ameachia ngoma yake mpya inayoitwa TOTO.

“Wakati mwingine unakuta mtu anatoa nyimbo ambayo hajaigharamia kwa chochote kwa kuwa tayari ana washikaji wengi watakao msaidia katika Video na hata Audio mwisho wa siku inatoka nyimbo mbaya au ambayo haina viwango” amesema Tundaman.