"Tulijiuliza kama tutaboa kweli" - Killy

Jumatano , 9th Jun , 2021

Good news kwa mashabiki wa Killy ambaye amerudi kimuziki baada ya kukaa kimya kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kuhama lebo ya Kings Music Records ya Alikiba na kuhamia Konde Gang ya Harmonize.

Msanii Killy kwenye studio ya East Africa Radio

Msanii huyo amesema kipindi anafanya maamuzi ya kuhama Kings Music ilikuwa ni kipindi kigumu cha maisha yake ya muziki hali iliyomfanya kujiuliza maswali mengi ikiwemo kama watatoboa kweli baada ya kufanya kitendo hicho.

"Kipindi ambacho tulihama Management ilikuwa ni kipindi kigumu sana ambacho sijawahi kukipitia kwenye maisha yangu kwa sababu ya maamuzi magumu niliyoyachukua, matusi yalikuwa mengi mpaka kuna muda tulikuwa tunajiuliza tutatoboa kweli" ameeleza Killy

Killy na Cheed wote walihama kwa Alikiba kwenda kwa Harmonize mwezi wa nne mwaka 2020, kwa sasa Killy amerudi na wimbo wake wa 'Roho' pia ana ujio wa Album yake mpya itakayotoka siku zijazo.