"Tulijisahau, tumetumia sana pesa" - Juma Nature

Jumatatu , 3rd Mei , 2021

Mkali wa 'chorus'  Juma Nature amewashauri wasanii wapya kwenye 'game' ya BongoFleva kwa kusema wakipata pesa waangalie vitu vya msingi vya kufanya na kuwekeza kwenye vitu vya maana kwa sababu muda haurudi nyuma.

Msanii Juma Nature

Akitoa ushauri huo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio Juma Nature amesema hata wao walipaswa kuwa matajiri wakubwa kwa sababu walishika sana pesa kipindi cha nyuma ila wakazitumia.

"Ninachomshauri msanii yeyote anayepata jina au anaetaka kutoka kwanza asiwe mzembe, majivuno, asibweteke na asiendekeze starehe kwa sababu zinafanya mtu akapaotea kabisa tena kwa dakika sifuri, wakipata pesa waangalie vitu vya msingi au fursa zakufanya muda haurudi nyuma" 

"Mimi dingi lao Naongea hivi kwa sababu nimeyaona mengi sana, sisi tulitakiwa tuwe watu wakubwa sana na nikizungumzia ukubwa sio wa jina bali ni utajiri, hapa katikati game ika-change halafu tulijisahau kidogo pesa tulipata mno ila tumetumia sana" ameeleza Juma Nature

Aidha amesema uzuri wa suala la kufanya sanaa haliihitaji elimu kwani ukikitumia vizuri kipaji chako kinaweza kukuingiza pesa nzuri ya kutengeneza maisha.