Tamasha la kampuni ya Tigo Kiboko Yao
Tamasha hili ambalo litaandika historia mpya ya burudani ya muziki nchini Tanzania litawakutanisha jumla ya wasanii 18 wakali hapa Bongo katika jukwaa moja, wakiwemo Weusi, AY, Mwana FA, Fid Q, Profesa Jay, Shaa, Vanessa Mdee, Jux, Ben Pol, Linah, Shilole, Isha Mashauzi, Khadija Kopa, Sikinde Band, Msondo Band, Yamoto Band, Christian Bella akiwa na Malaika Band, bila kusahau Ali Kiba pamoja na Diamond Platinumz.
Kama bado hujapata tiketi yako, jiunge na kifurushi cha wiki ama mwezi kupitia line yako ya Tigo, na ukiwa kati ya watu 6,000 wa kwanza kununua vifurushi katika siku, Tigo watakutumia ujumbe kukujulisha na ujumbe huo utaujibu kwa neno Kiboko Yao ili kuweza kutumiwa code namba, ambayo itakuwa ndiyo tiketi yako ya kuingia katika tamasha hili. Kumbuka, Hii ni Tigo Kiboko Yao.