Ijumaa , 30th Jan , 2015

Mwigizaji na mtayarishaji filamu Timothy Conrad a.k.a TICO, ameweka wazi juu ya ujio wa tamasha kubwa la Filamu litakalosimama kwa jina Timamu African Film Festival.

Mwigizaji na mtayarishaji filamu wa nchini Tanzania Timothy Conrad a.k.a TICO

TICO amesema kuwa lengo la tamasha hili ni kuzileta pamoja kazi za filamu za Afrika na pia kutoa tuzo kwa kazi ambazo zitakuwa zimefanya vizuri.

Tayari tamasha hili limekwishaanzishwa na kusajiliwa nchini Marekani, na taratibu zake za usajili zinakamilika pia hapa nchini ambapo kuanzia mwezi wa pili wasanii hapa nyumbani wataweza kuwasilisha kazi zao za filamu, matarajio yakiwa ni kufanya tamasha hili ifikapo mwezi wa 9 mwaka huu.