Jumapili , 13th Jul , 2014

Muigizaji nyota wa filamu nchini Marekani Terrence Jenkins ambaye ametua Jijini Dar es Salaam kufuatia mualiko wa Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kuendesha semina maalum kwa wasanii amefurahishwa na mapokezi makubwa ya mashabiki nchini.

Muigizaji filamu wa nchini Marekani, Terrence Jenkins

Terrence pia aliungana na mashabiki na wasanii mbalimbali nchini Tanzania katika kupremier filamu yake mpya iliyobatizwa jina 'Think Like A Man Too' ikiwa ni toleo la sehemu ya pili.

Muigizaji huyo nyota ameongea na eNewz kuhusiana na kuendesha semina hiyo ya kuwasaidia wasanii mbalimbali nchini katika kuendeleza vipaji vyao na jinsi ya kujitangaza zaidi tasnia ya burudani kimataifa.