Ijumaa , 23rd Nov , 2018

Tanzania imeonekana kupewa heshima kubwa kwenye jukwaa la filamu nchini Marekani 'Hollywood', baada ya kampuni maarufu ya kutengeneza filamu ya Disney, kuweka picha za mlima Kilimajaro kwenye filamu mpya ya 'The Lion King' ambayo inatarajiwa kuachiwa Julai 2019.

Filamu hiyo ambayo inatengenezwa na Wall Mat Disney inaongozwa na mwongozaji maarufu wa filamu za 'animation', Jon Favreau, ambaye pia ameongoza filamu kama 'The Jungle Book' na 'Iron Man'.

Kwenye video fupi ( Trailer) ya filamu hiyo ambayo imetoka jana Novemba 22, 2018, imeanza kwa kuonyeshwa ndege wakiruka mbugani kisha kuonyeswha mlima Kilinjaro, jambo ambalo linaweza likawa fursa nzuri kwa Tanzania kuzidi kutangazwa vivutio vyake kimataifa.

Kingine kikubwa kwenye filamu hiyo ni kukutana kwa mastaa kibao wa Hollywood, ambao wametia sauti za wanyama hao kama Beyonce aliyeigiza kama Nala, Rapper wa Marekani mwenye hit song ya 'This is Amrica', Childsh Gambino ambaye ameigiza kama Simba na wengine kibao.

Washiriki kwenye filamu ya The Lion King