
Ruben Amorim - Kocha wa Klabu ya Manchester United
Kwa mujibu wa Manchester Evening ni kuwa United wanataka kuwauza kabisa wachezaji watatu Marcus Rashford, Antony na Jadon Sancho ambao kwa sasa wako kwa mkopo katika vilabu vingine baada ya kukosa nafasi Old Trafford. Pesa zitakazopatikana kutokana na mauzo hayo zitatumika kumsajili mshambuliaji mpya.
Kiungo, Casemiro pia atauzwa huku Jonny Evans na Tom Heaton wanatarajiwa kutangaza kustaafu mwisho wa msimu huu, Christian Eriksen na Victor Lindelof wakitarajiwa kuondoka. Mustakabali wa Altay Bayindir haujafahamika.
PSV pia wana chaguo la kumsajili beki wa kushoto Tyrell Malacia kwa mkataba wa kudumu huku Utd wakiangalia namna ya kuachana na Luke Shaw kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.