Msanii wa Taarab Mzee Yussuf
Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari Mzee Yussuf amesema wamekuja na kauli mbiu yao ambayo inasema hatuna dogo kwa sababu hawataki kufanya jambo lolote kwa udogo bali kwa ukubwa ili kuwafikia watu zaidi.
"Nataka niifanye Taarab kama wanavyofanya wenzetu wanavyopeleka vitu vyao kwenye 'Digital Platfrom' maana dunia ndiyo ipo huko sasa hivi, Pia nataka Taarab ipokee tuzo za nje ya nchii hii mpaka kila mtu aseme kweli tumeamua"
Aidha Mzee Yussuf ameongeza kusema "Pia nataka kubadilisha zile style tulizozizoea kwenye Taarab na kuziongezea utamu zaidi kwa sababu kama kuimba tunaweza hata tukiamshwa usiku wa manane, ila kwenye video kuna mahali tunafeli"
Ikumbukwe msanii huyo alitangaza kuacha muziki miaka mitano iliyopita ila kutokana na shida za kimaisha ameamua kurudi tena.