Alhamisi , 16th Jul , 2015

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Joseph Mbilinyi aka Mr. Sugu ambaye ni mwana Hip Hop mkongwe amepata mpinzani aliyetangaza nia ya kuwania kiti hicho ndani ya chama hicho.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,(CHADEMA) Mh. Joseph Mbilinyi aka Mr. Sugu

Mpinzani huyo wa Mh. Sugu ni mwaandishi wa habari ambaye ni mwakilishi wa kampuni ya magazeti ya Free Media mkoani Mbeya, Christopher Nyenyembe ambaye amechukua fomu na kusema iwapo atapata ridhaa ya kupeperusha bendera ya CHADEMA atakuwa jirani na wananchi kusikiliza vipaumbele na kuahidi kuvitekeleza kwa asilimia 100.

Nyenyembe aliwahi kuwania nafasi ya Ubunge jimbo la Mbeya mjini katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 na kushika nafasi ya tatu kwa tiketi ya CHADEMA, akitanguliwa na Mh. Sugu.