Alhamisi , 14th Mei , 2015

Staa wa muziki STL ambaye mbali na muziki pia kwa sasa ameshikilia kampeni ya kutangaza mavazi ya kiafrika aliyoyapatia jina Vaa Kiafrika, amepata nafasi ya kuonesha mitindo hiyo katika onesho kubwa la mitindo huko nchini Norway.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Stella Mwangi aka STL

Chini ya kampeni yake ambayo ameipatia jina Vaa Kiafrika, staa huyo wa nchini Kenya alitumia wanamitindo wanne ambao walivaa mitindo yenye nakshi ya kitenge, vazi ambalo asili yake ni bara la Afrika.

STL kwa sasa amejijengea jina kwa upande wa mitindo, akitumia pia kurasa zake za kijamii kutangaza ufahari na uzuri wa mavazi mbalimbali ambayo yamebuniwa na kutumia malighafi ambayo ni kutoka Afrika.