Staa wa filamu Wema Sepetu na mchezaji wa Yanga Carlinhos
Steve Nyerere ameeleza hilo baada ya kusambaa kwa picha mitandaoni kati ya Wema Sepetu na Carlinhos ikiwaonyesha wakiwa pamoja.
"Uongozi wa Yanga popote mlipo mtatua mashabiki wenu jamani, tunanunua mchezaji kwa bei kubwa, tunampokea uwanja wa ndege kwa mbwembwe, dakika ya mwisho hali ndiyo hii, tafadhali kuhujumu uchumi sio kuiba hela tu hata hili mnaloliona, kuna watu watawajibika Wema Sepetu endelea nakwambia" ameandika Steve Nyerere
Aidha Steve Nyerere ameongeza kuwa "Unatuharibia mchezaji mimi kwa hili na huo udugu utakufa wallah, nakwambia tena huoni bado mtoto huyu sasa hivi utasikia gauti gauti, wana Yanga sio la kucheka hili mtoto anapotea huyu"