Skales aitaka collabo na Nandy

Jumanne , 8th Jun , 2021

Msanii wa Nigeria, Skales aitaka collabo na The African Princess ‘Nandy’ hii ni mara baada ya kuacha comment kwenye moja ya post za msanii huyo wa Bongo Fleva.

Msanii Skales

Huku akisema “Studio wen you come” (Ukifika ni Studio) na kisha Nandy akajibu kwa kusema “Yeees my brother” (Ndio kaka yangu).

The African Princess inaonesha yupo njiani kuelekea nchini Nigeria kwa shughuli za kimuziki akiwa ameambatana na meneja wake Moko Biashara.

Skales ni moja kati ya wasanii ambao shughuli zake za kimuziki kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki zinasimamiwa na lebo ya muziki ya msanii Harmonize ambayo ni Konde Music Worldwide.