Mwandaaji wa muziki C 9
Akizungumza na Enewz C9 alisema kuwa hawezi kusahau kuwa aliumwa sana hadi akashindwa kufanya kazi zake kwa muda mrefu huku akiwa hajui anaumwa nini.
Amesema hata alipokwenda hospitali baada ya kufanyiwa uchunguzi alielezwa kuwa hakuna tatizo lililokuwa likionekana.
“Nilikuwa najisikia naumwa vibaya nilikuwa siwezi kugusa hata key-board kabisa, kuna kipindi najisikia vizuri lakini nikifikiria kufanya kazi na mtu fulani au kitu fulani najisikia naumwa siwezi kuingia studio, ikanibidi nimrudie Mungu yaani niliona vitu vingine hospitali vinashindikana lakini kwa Mungu vinawezekana na mpaka sasa nipo freshi”, alisema C9.