Jumanne , 8th Jul , 2025

CEO wa Free Nation Nay Wa Mitego anasema hataki mtoto wake wa kike aende kupanga na kuanza kujitegemea kimaisha hata kama awe anafanya kazi na anapokea mshahara mkubwa.

Nay Wa Mitego ametufahamisha hilo kwa kushea ujumbe huu kupitia Insta Story yake unaosema ........"Moja kati ya kitu sitotaka kusikia ni mtoto wangu wa kike kwenda kujitegemea yani kupanga, hata kama awe anafanya kazi wapi na mshahara mkubwa vipi ni nyumbani tu" Ameandika Nay

"Kutoka nyumbani labda aende kwa mumewe na ndoa ikimshinda ni kurudi nyumbani ale, alale afurahie maisha. Wa kiume muda wowote tu akajitegemee akiamua na wakiume kukaa kwangu mwisho miaka 17". Ameandika Nay