Alhamisi , 5th Mar , 2020

Mkongwe wa Bongofleva Dully Sykes  ni mmoja wa wasanii ambao walikuwa wanakashfa ya kupenda wanafunzi, kupitia EATV & EA Radio Digital amesema ni kweli kipindi  hiko alikuwa anapenda wanafunzi lakini hata yeye alikuwa mwanafunzi pia.

Picha ya msanii wa BongoFleva Dully Sykes

Dully Sykes amesema sasa hivi hana stori na watoto wa kike,ila kwa wakati ule anapata kashfa hizo hata yeye alikuwa ana umri mdogo wa makamo ya kiuwanafunzi kwa hiyo haikuwa shida kuwapata.

"Unajua sio kila anayebaka chanzo anakuwa ni yeye pengine chanzo ni mbakwaji, kwa kipindi kile  watu wanasikia napenda wanafunzi  hata mimi nilikuwa mwanafunzi pia japo nilikuwa sipo shule, lakini kwa makamo yale yalikuwa ya kiuwanafunzi kwa hiyo kuwapata haikuwa mbaya" amesema Dully Sykes.

Aidha Dully Sykes ameendelea kusema "Nilivyokuwa mtu mzima nikaanza kuchukua watu wazima wenzangu hadi nikapata nao watoto kabisa na sijawahi tena kuchukua videnti" ameongeza.