Alhamisi , 25th Aug , 2016

Msanii Man Fongo ambaye ni bingwa wa kuipiga singeli studio na mitaani, ametoa sababu ambayo ilifanya muziki huo uanze kwa kukwama, na kuchelewa kutoka.

Msanii Man Fongo

Akizungumza na Planet Bongo ya East AFrica Radio, Man Fongo amesema muziki huo ulikuwa umeshaaminika ni wa kihuni, kwani hata mitindo yake ya uchezaji ilikuwa siyo ya kufaa kwa jamii, na pia ilikuwa ni hatari kwa kuwa watu wengine hucheza na silaha.

"Muziki ulikuwa bado mchanga na walikuwa hawajaupokea, ulikuwa unonekana wa kihuni, zamani ilikuwa wanacheza wahuni tu kati, ukicheza uwe na roho ngumu hasa, lakini sasa hivi kina mama, watoto, masela na kila mtu anacheza, mpaka tunaingia studio kubwa", alisema Man Fongo.

Man Fongo aliendelea kusema kuwa sababu iliyoufanya muziki huo uonekane wa kihuni ni kutokana na kipindi hicho hawakuwa na uwezo wa kuingia studio kubwa na kuurekodi, na kuupa hadhi nzuri kwa jamii.