
Dogo Janja ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kwamba kitendo cha yeye kushabikia chama fulani cha siasa hajalazimishwa na mtu yeyote, huku kusisitiza suala la amani na kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi.
"Kama mimi chaguo langu na mtu ambaye ninampenda hakuna mtu ambae anaweza akanipangia, mi siwezi kuwa na ukanda, na wala siwezi kuwa na ukabila, sina ukaskazini, kama Mtanzania mwisho wa siku kuna maisha baada ya uchaguzi, watu waishi kwa amani", alisema Dogo Janja.
Dogo Janja aliendelea kwa kusema kwamba wote ni Watanzania tunaongea lugha moja, hivyo haina haja ya kugombana.