Jumatano , 15th Apr , 2015

Nyota wa muziki wa Injili hapa Tanzania, Christina Shusho amemwagia sifa msanii mwenzake, Rose Mhando kutokana na uwezo mkubwa katika kipindi hiki ambacho aina ya maonesho anayofanya yamekuwa yakizua mitazamo tofauti kwa mashabiki.

Wasanii wa nyimbo za injili Rose Muhando na Christina Shusho

Katika mahojiano tuliyofanya naye, Shusho ambaye hivi sasa yupo jijini Nairobi nchini Kenya amesema kuwa Rose ni msanii wa kipekee na mbunifu, tofauti na wengi wanavyomtafsiri, na hapa anaeleza zaidi.