Jumanne , 14th Jul , 2015

Mwimbaji nyota wa muziki wa injili nchini Christina Shusho ametoa wimbo wenye lengo la kuhimiza amani haswa katika wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu nchini.

mwimbaji wa muziki wa injili nchini Tanzania Christina Shusho

Christina ameongea na eNewz kuwa hii ni nafasi kwa watanzania wote kutambua kuwa bila amani hatutoweza kuwa na maendeleo katika nchi na amezungumzia pia mipango yake ya kuandaa kichupa cha wimbo huo mpya uliobatizwa jina 'Tanzania Kwanza' utakaoshirisha viongozi, wachungaji, watu na wadau mbalimbali.