Alhamisi , 22nd Dec , 2016

Msanii wa bongo fleva Shilole maarufu kama Shishi Trump amefunguka na kusema kazi yake ya upishi ambayo sasa anaifanya inamuingizi kiasi cha hadi shilingi laki tano kwa siku. 

Shilole akiwa kwenye kazi yake ya Mama Lishe

Shilole alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio na kudai hata kama siku akiachana na muziki yeye ataendelea na biashara hiyo ya upishi kwani licha ya kumuingizia kipato, ni kazi ambayo yeye mwenyewe anaipenda kufanya.

"Unajua mimi niliaangalia kila msanii anataka kuwa na duka la nguo, saloon, nikaona bora nifanye biashara ya chakula kwani watu hawawezi kununua nguo kama hawajala chakula, watu kila siku lazima wale chakula, nikajiangalia mimi mwenyewe hata kama sitakuwa na pesa lazima nitakula hivyo nikaona huku ndiko, lakini pia kwangu mimi ni kama hobi kwani hata mama yangu alikuwa anafanya kazi ya Mama Ntilie. Kiukweli nashukuru Mungu kwa kazi yangu hii ya upishi kuna wakati naingiza mpaka laki tano kwa siku hivyo hata nikiacha kufanya muziki nitaendelea na biashara yangu hii kwani naipenda" alisema Shilole.

Tags: