Ijumaa , 25th Oct , 2019

Msanii wa Muziki wa BongoFleva Shilole, amesema akikutana na muigizaji Mwijaku,  kitu pekee atakachomshauri ni muigizaji huyo awe makini katika mambo anayoyafanya, kwa kuwa yeye sasa ni mume wa mtu na na anafamilia inayomtazama.

Shilole ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI,  kinachoruka kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8 : 30 Mchana hadi saa 9 : 30 Alasiri, ambapo alitakuwa kutoa ushauri kwa Mwijaku pamoja na muigizaji Menina.

Shilole amesema kuwa "namshauri Menina akaze moyo, najua hakutugemea kuvujisha vile vitu vyake, kwanza mimi namuona ni shujaa mwingine angejiua, ni bahati mbaya tu ile imetokea''.

"Mwijaku yeye nimtu mzima na Mke inabidi apunguze spidi ya 4G, yaani apunguze kidogo sana." amesema Mwijaku.

Aidha Msanii huyo amemshushia sifa mwanamuziki Gigy Money, na kusema msanii huyo kwa sasa amekuwa ni mfano mzuri kwenye jamii, ambaye anafaa kufuatwa na kila mtu.