Jumatano , 8th Oct , 2014

Msanii wa muziki nchini Uganda, Sheeba Karungi, ameweka wazi kuwa asingekuwa msanii wa muziki, angekuwa katika shughuli za Kamera au muongoza video kutokana na uwezo mkubwa wa maoni ya namna kitu kinavyotakiwa kuwa.

msanii wa nchini Uganda Sheeba Karungi

Sheeba amesema kuwa, kila wakati anapokuwa Studio, akimaliza kurekodi hufanya kazi ya kutengeneza picha ya namna video ya kazi hiyo itakavyotakiwa kuwa kutokana na uwezo alionao.

Sheeba amesema kuwa, video zake zinakuwa na utofauti sana kutokana na uwezo wake huu ukiunganishwa na mchango wa muongozaji wa video husika.