Jumatatu , 24th Mei , 2021

Mwanamuziki Shaa anakaribia kufikisha miaka mitano bila kuachia ngoma yoyote licha ya kutowahi kutangaza kuacha kufanya muziki na mara ya mwisho alitoa wimbo mwezi Julai 14, 2016 na uliitwa ‘Sawa’.

Msanii Shaa

Shaa alijizolea umaarufu mkubwa kupitia kazi zake kama ‘Sugua gaga, Shoga na Crazy’ huku akiwa ni msanii aliyefanikiwa kusimamiwa na msanii AY chini ya mwavulii wa Unity Entertainment na Mkubwa na wanawe kwa nyati tofauti.

Licha ya mzazi mwenzie ‘Master J’ mara kadhaa kukiri kuwa Shaa alifanikiwa kutengeneza kiasi kikubwa sana cha fedha kupitia muziki wake lakini ghafla tu aliamua kukaa kimya huku akiendelea na shughuli zake za kifamilia na sasa ni Mama wa mtoto ‘Niabella’.