Jumanne , 4th Aug , 2015

Kundi la muziki la Sauti Sol la nchini Kenya, limetajwa kuwa kundi ambalo linatengeneza pesa nyingi zaidi kutokana na malipo ya mirahaba ya matumizi ya kazi zao, orodha ambayo mara nyingi ilikuwa ikiongozwa na wasanii wa muziki wa injili Kenya.

Kundi la muziki la Sauti Sol la nchini Kenya

Katika orodha hiyo mpya kwa kufuata viwango ambavyo mastaa hawa wanaingiza, nafasi ya pili inashikiliwa na Bahati, akifuatiwa na Lady Wanja, Willy Paul na Mum Cherop ambao wanakamilisha tano bora.

Orodha ya mwaka huu pia inakuwa ni ishara ya mabadiliko makubwa katika muziki Kenya, kutokana na kazi nzuri bendi ya H_Art, Rapa Rabbit ikiwa ni majina mengine yaliyong'ara katika orodha hiyo.