Kundi la muziki la Sauti Sol la nchini Kenya
Pembeni ya suala zima la utamaduni, kundi hili limegusa mioyo ya mashabiki wake kwa namna ya kipekee pia kwa kuachia saa 48 za awali za albam hiyo mtandaoni kwa mashabiki kujipakulia bila gharama yoyote, ikiwa na rekodi 15 zenye mvuto na ladha ya kipekee.
Mwishoni mwa wiki, wadau na watu mashuhuri walipata nafasi ya kusikiliza rekodi za albam hiyo katika hafla maalum, ikiwa ni mkakati wa kundi hilo kuunganisha nguvu na wasanii wengine Afrika kuonesha uwezo mkubwa wa bara hili katika sekta mbalimbali.