Wanamuziki wa kundi la Sauti Sol nchini Kenya
Katika jarida hili, kutoka Sauti Sol, Bien-Aimé Baraza, Polycarp Otieno, Willis Austin Chimano pamoja na Delvin Mudigi wamejaribu kuonyesha ladha na mitoko yao ya kipekee katika mitindo, na kuwaachia mashabiki nafasi ya kuamua ni nani ametokelezea zaidi ya mwenzake.
Wasanii hawa wamekuwa na vipaji vya aina yake katika sanaa ya muziki, na hata mionekano yao kila siku imekuwa ikionyesha umakini mkubwa kimitindo kwa uchaguzi wa mavazi ambayo wamekuwa wakivaa.