Ijumaa , 29th Mei , 2015

Mastaa wa muziki wa Bongo fleva pamoja na mashabiki wamekuwa na maoni tofauti ya huzuni kufuatia taarifa za kufika mwisho kwa show mahiri kabisa ya Planet Bongo siku ya kesho, mtangazaji muanzilishi wa show hiyo Salama Jabir atakiendesha.

mtangazaji wa kipindi cha Mkasi cha EATV Salama Jabiri

Kwa heshima ya maelfu ya wapenzi wake, mtangazaji muanzilishi wa shoo hiyo Salama Jabir atakiendesha.

Kutoka katika mahojiano ambayo eNewz tumefanya leo, kwa niaba ya wasanii, AY na vilevile TID ambao wapo katika muziki kitambo, wameelezea kuhuzunishwa na taarifa za kufa kwa show kubwa kama hiyo huku mzee wa Commercial akiwa haamini akihisi kuna ujio wa kitu kizuri zaidi.

Kwa upande wa pili pia mashabiki wa show hii ya aina yake wakawa na haya ya kusema kuhusiana na mwisho wa Planet Bongo.