Rozay apata leseni baada ya miaka 45

Jumatatu , 13th Sep , 2021

Licha ya kujigamba kuwa na utitiri wa magari ya kifahari nyumbani kwake, Rapper Rick Ross hakuwahi kuwa ameruhusiwa kisheria kuendesha gari yoyote kwa kukosa leseni ya udereva.

Picha ya Msanii Rick Ross

Hivi sasa bosi huyo wa Maybach Music Group amepata leseni akiwa na umri wa miaka 45 baada ya kipindi cha karibu miongo mitatu kupita, ambapo ushawishi mkubwa amesema aliupata kutoka kwa Mama na Dada yake ambao walikuwa wakimsumbua siku zote kwasababu wao ndio walikuwa wakimuendesha mara kadhaa.

Rozay amef ungua hayo kwenye mahojiano yake hivi karibuni wakati akikitangaza kitabu chake kinachoitwa "The Perfect Day to Boss Up".