Alhamisi , 9th Nov , 2023

Vita ya maneno na spana bado zinaendelea huko mtandao wa X baada ya rapa Wakazi kumchana Roma Mkatoliki akimwambia sio mwanaharakati kama anavyojinasibu.

Picha ya rapa Wakazi

Wakazi amefunguka hilo baada ya kuandika kuwa 

“Roma labda uwadanganye wapwa ila sio sisi watu wazima wenzako.
Sio mwanaharakati kiivyo kama unavyojinasibu”

“Wewe ni Msanii wa kusema vitu for shock value, upate reaction kisha Media zikupige na kukupa shows”.

“Mzee wa Hit Song wakati hit zenyewe wanazo kina Darassa, AY, Chid Beenz”.

Vita yao hiyo ya maneno inaenda kumaliza mwaka sasa na ilianzia mtandao wa X kwa kila mmoja kushea maoni yao kuhusu muziki na uwezo wa binafsi kama wasanii.