![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2016/08/02/gggggggggggggggggggggggggggggggggggggggg.jpg?itok=2pI3ul92×tamp=1473878312)
Majaji wa shindano la Dance100%
Akizungumza na EATV kuhusu mwendelezo wa shindano hilo mratibu wa shindano hilo Bhoke Egna amesema shindano litaelekea katika nafasi muhimu ambapo makundi yote yanajipanga kwa ajili ya mtoano wa robo fainali.
''Robo fainali inafanyika tarehe 13 .8.2016 katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na shindano hilo kutakuwa na zawadi mbalimbali kutoka kwa Vodacom na Coca- Cola''. Amesema Bi. Bhoke
Aidha siku hiyo yataaga mashindano makundi matano na kubakia makundi 10 ambayo yataingia katika hatua ya mchuano wa nusu fainali.
![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/2016/08/02/99999999999999999999999999999999999999999ufjm n.jpg?itok=2EjfavA8)