Jumatatu , 2nd Nov , 2015

Nyota wa muziki kutoka nchini Kenya, Ringtone anajipanga kwa ajili ya kuisimamisha taasisi ambayo itakuwa ikiendesha shughuli zake za kuwafikia vijana na kuwasaidia kutimiza ndoto na mipango yao mbalimbali katika maisha.

Nyota wa muziki kutoka nchini Kenya, Ringtone

Mpango huo unakuja baada ya msanii huyo kuonekana mara kwa mara katika harakati za kulifikia kundi hilo katika jamii na kutoa msaada wake, ikiwepo pia wasanii ambao wamekuwa mstari wa mbele kupigania haki zao mbalimbali ikiwepo hakimiliki ya kazi zao na mirahaba.

Kupitia taasisi hiyo, star huyo ataweza kutekeleza majukumu yake kwa njia rasmi na kuendeleza ndoto yake ya siku zote ya kuwa na mchango chanya kwa jamii inayomzunguka.