Jumatano , 15th Nov , 2023

Kutoka Nigeria msanii Rema amemtumia ujumbe wa kumshukurua The African Giant Burna Boy kwa kumpa nafasi ya kupanda jukwaani miaka miwili iliyopita kabla hajawa mkubwa kimuziki kama sasa hivi.

Picha ya Rema kulia na Burna Boy kushoto

Rema ameshea ujumbe huo kupitia Akaunti yake ya mtandao wa X kwa kupost picha yake na Burna Boy wakiwa stejini na kuandika

"Kabla sijapanda jukwaani, nataka kusema asante sana Burna Boy kwa kunileta jukwaani miaka 2 iliyopita. Leo ni zamu yangu ya kushinda hatua hiyo hiyo na ninatamani ungekuwa hapa kushiriki wakati huu nami. Bila kujali, ninashukuru kwa motisha".

Wasanii hao wote wamehusika kufanya shows za matukio makubwa kwenye soka duniani mwaka huu kwa mfano Burna Boy kuperforme fainali ya UEFA na Rema kuperforme kwenye tuzo za Ballon D'or.