Jumamosi , 28th Jun , 2014

Boss wa lebo ya muziki ya Grandpa ya nchini Kenya, hatimaye amekamilisha rasmi taratibu za kiutamaduni za ndoa yake na kuwa tayari kuanza rasmi maisha mapya na mkewe, na hii ikiwa ni baada ya sherehe kubwa ya harusi yake iliyofanyika mwezi uliopita

Refigah

Hii ni kupitia taratibu za kimila za asili ya Refigah ambayo ni kutoka huko Kaskazini mwa Sudan, Jamii ya waNubia ambapo shughuli yenyewe uhusisha mama wa bwana harusi kutoa zawadi kwa rafiki wa mwanae kwa ushirikiano walioonesha wakati wa harusi.

Shughuli hii imepata kuhudhuriwa na watu mbalimbali wa karibu na Refigah ikiwepo timu ya Grandpa ikiongozwa na msanii wake mkali, DNA.

Mama wa Refigah akikabidhi marafiki zake zawadi