Alhamisi , 16th Jun , 2016

Msanii wa muziki wa bongo fleva anayekuja kwa kasi Raymond wa WCB amefunguka ndani ya Enews kuhusiana na wanamuziki ambao wanaachia ngoma ambazo walimshirikisha zamani.

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Raymond

Amesema kuwa kwa sasa yeye yupo kwenye uongozi wa WCB hivyo uongozi wake hauzitambui kabisa nyimbo zote alizoshirikishwa kabla ya kujiunga WCB.

Akizungumzia wimbo wa cheza kidogo wa msanii KAMIKAZE ambao unafanya vizuri kwa sasa Raymond anasema huo wimbo hakushirikishwa kwa ajili ya kuimba bali alikuwa akimuelekeza msanii mwenzake KAMIKAZE melodi na jinsi ya kuimba wimbo huo.

Hali iliyopelekea hadi kuingiza sauti na kurekodi, lakini alishangaa kuona Kamikaze ameuachia wimbo huo kuusambaza kama kwa madai kuwa walifanya 'kolabo'

Hata hivyo Raymond amesema hayupo tayari kabisa kuonekana katika video ya wimbo huyo licha ya KAMIKAZA kusema hana tatizo kabisa na uongozi wa Raymond.