Ray Kigosi aja na mpya

Saturday , 18th Nov , 2017

Msanii wa filamu bongo Vicent Kigosi maarufu kama Ray, leo amekuja na mpya baada ya kusema yale aliyokuwa akiyafanya utotoni alipokuwa shule.

Akipiga stori na Big Chawa wa Planet Bongo ya East Africa Radio, Ray amesema alipokuwa mtoto alikuwa mtukutu na kukaa nyuma kabisa ya darasa kwa wale wanafunzi wanaojulikana maarufu kwa kupiga kelele, (backbencher) na kuwa wa kwanza kutoka nje kabla ya muda muafaka kufika.

Pamoja na hayo Ray amesema alipohitimu elimu ya sekondari alifeli na kupaa division four, lakini kitendo hiko hakikumkatisha tamaa na kufeli maisha.

Msikilize hapa chini